Dante: Nitapigania namba Yanga

08Jun 2016
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe
Dante: Nitapigania namba Yanga

BEKI mpya wa klabu ya Yanga, Andrew Vicent 'Dante' amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo akitoka Mtibwa Sugar.

BEKI mpya wa klabu ya Yanga, Andrew Vicent 'Dante'


Dante, mmoja wa mabeki bora wa kati nchini, hivyo kujiunga kwake Yanga ina maana atawania nafasi hiyo na Kelvin Yondani, Nadir Haroub 'Canavaro', Pato Ngonyani na Vicent Bossou.


Kusajiliwa kwa Dante kutaongeza ushindani kwenye safu ya ulinzi ndani ya kikosi hicho cha Yanga kinachojiandaa na hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho.


Dante, aliiambia Nipashe kuwa anajua changamoto anazokwenda kukutana nazo ndani ya Yanga, hata hivyo amejipanga vizuri.


Alisema kuwa moja ya mbinu atakayotumia ni kuhakikisha anatumia vizuri kila nafasi atakayopewa kucheza.


"Kila sehemu kuna changamoto yake, nitapambana kuhakikisha napata nafasi kwenye kikosi cha kwanza," alisema beki huyo aliyeonyesha kiwango kizuri akiwa Mtibwa.