Baada ya kusaini makubaliano hayo, ushirikiano wa NMB na Yanga utalenga maeneo yafuatayo:
Kutumia mtandao mpana wa NMB unaojumuisha matawi zaidi ya 228 kote nchini kufanya usajili wa wanachama na mashabiki wa Yanga, wakiwemo wenye umri chini ya miaka 18. Kadi hizo maalum zitakua na nembo za Yanga na NMB.
"Mwanachama wa Yanga atalipia sh.34,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga (Shilingi 5,000 ni malipo ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na sh.24,000 ni ada ya Mwanachama kwa mwaka mzima).
Kadi za mashabiki ambao sio wanachama - Malipo yatakua sh.22,000 tu (shilingi 5,000 ni ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 12,000 ni ada ya shabiki kwa mwaka mzima).
Kadi hizo hazitakua za uanachama/ushabiki tu, pia zina uwezo wa kufanya kazi kama kadi ya Benki! Unaweza kufanya miamala yote ya kibenki ikiwemo kuiwekea pesa, kutoa hela katika ATM na kufanya malipo mtandaoni na katika vituo vya malipo (POS).
Wanachama wanaweza kupata kadi za Malipo ya Kabla (Prepaid Card) ambayo huitaji kuwa na akaunti nasi na kufanya malipo kwa kupitia mtandao au kwenye Point of Sales (POS).
Wanachama na mashabiki watanufaika na huduma na ofa mbalimbali za NMB ikiwemo mikopo isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta) na punguzo la bei wakifanya malipo kupitia NMB Lipa Mkononi (QR).
Benki ya NMB itawezesha matawi ya Yanga zaidi ya 900 nchi nzima kutoa huduma za uwakala wa NMB.
Mbali na huduma za uanachama, NMB itaanzisha Bima ya Mwananchi ambayo itakua na gharama nafuu.
Makubaliano haya yamesainiwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB - Filbert Mponzi na Rais wa Klabu ya Yanga – Injinia Hersi Said na kushuhudiwa na viongozi wengine wa Benki na Klabu.
Usajili huo utaanza rasmi Julai 10, 2023 kwenye matawi yote ya NMB. Tembelea tawi la NMB lililo karibu yako kupata maelezo zaidi.










