Baraka da Prince, Najma safi kabisa

17Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Baraka da Prince, Najma safi kabisa

MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Baraka da Prince, amesema huku akitarajia mtoto na na mpenziwe Najma, kitendo cha kumtambulisha kwa wazazi wake amewazima wale wote waliokuwa wakijigonga kwake na kutangaza kwamba yeye ni mchumba wao.

baraka prince

Alisema kuwa tayari amejifunga na hatarajii kubadili msimamo wake kwa Najma, kwa madai kwamba ameona ndiye anayefaa kuwa mke wa kuoa kuliko hao waliokuwa wakijitangazia ufalme.

"Nimejipa mwaka mmoja na kisha nitafunga ndoa kwani nina uhakika kipindi hicho kinanitosha kumjua kiundani zaidi mchumba wangu, hivyo hao wengine wahesabu kuwa wameumia," alisema Baraka.

Miongoni mwa watu waliodai kuwa ni wachumba wa Baraka ni msanii wa filamu Nisha, ambaye aliwahi kusema kuwa amewekea ulinzi mkali za nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya.

Hata hivyo, likaibuka suala la umri kwamba Nisha ni mkubwa kuliko Baraka, lakini yeye (Nisha) akadai kuwa mapenzi ya sasa hayajali umri ili mradi wawili wawe wamekubaliana.

Baadaye Nisha alimkana Baraka akidai hana uhusiano naye, hatua ambayo iliwashangaza wengi kwamba alikuwa hakumbuki kile ambacho aliwahi kukisema kuhusu uhusiano wao!