Akizungumza baada ya mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Kitambi alisema kama wangeshinda mabao 2-0, wangekwenda ugenini kucheza mfumo ambao wanaamini ungewasaidia kusonga mbele, lakini bao hilo litawafanya kwenda kutafuta ushindi na si kuzuia.
Hata hivyo, aliwapongeza wachezaji wa Azam kwa kupigana kiume na kupata ushindi.
Kitambi pia alisema kukosekana kwa Shomari Kapombe kwenye mchezo huo pia ulikuwa pigo kubwa na kusababisha kubadilisha mfumo mzima wa uchezaji.
"Kwa asilimia 70 Kapombe ametuathiri mfumo wa timu na imebidi kubadilishe na kweli umeleta matunda pia, ingawa kukosekana kwake ni pigo.
Pamoja na hayo, kocha huyo alisema kuwa kuna utofauti kati ya wachezaji wa timu za Tanzania na timu za wenzetu
hususan kutoka Afrika Kaskazini kama alivyoona kwenye mechi mbili, ikiwemo ya Yanga dhidi ya Al Ahly.
"Wenzetu wakipata mpira wanatulia, tofauti na timu zetu, hivyo inabidi tubadilike," alisema.
Azam inahitaji sare yoyote ile ugenini ili kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
Imeandikwa na Adam Fungamwango na Renatha Msungu










