Man U wakana kumlazimisha LVG kujiuzulu

27Jan 2016
Nipashe
Man U wakana kumlazimisha LVG kujiuzulu

KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal hakuombwa kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kipigo cha nyumbani cha bao 1-0 kutoka Southampton mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka klabu hiyo zilizoripotiwa na Reuters.

louis van gaal

Awali, magazeti ya Uingererza, alikiwamo The Guardian liliandika kuwa Mwenyekiti Mtendani wa Man United, Ed Woodward, alimshawishi kocha huyo raia wa Uholanzi kujiuzulu nafasi hiyo baada kipigo hicho.
Mashabiki wa United waliwazomea wachezaji wao mwishoni mwa mchezo, huku Van Gaal akisema walikuwa sahihi kufanya hivyo.
Woodward alimtaka Van Gaal kuzungumza na familia yake kabla ya kuamua hatima yake United, liliandika gazeti hilo
Kocha huyo alirudi nyumbani Uholanzi ili aweze kushiriki siku ya kuzaliwa ya binti yake Jumapili wiki hii.
Van Gaal anatarajia jana kufanya mazungumzo na mapya na mamlaka za juu za United baada ya kurejea kwenye mazoezi ya timu hiyo.
Kipigo hicho kutoka Southampton kimeiacha United katika nafasi ya tano kwenye msimamo, kikiwa nyuma kwa pointi 10 kutoka kwa wanaoongoza Leicester City.