Waziri ataja sababu usitishaji uchimbaji makaburi Shakahola

21May 2023
NAIROBI
Nipashe Jumapili
Waziri ataja sababu usitishaji uchimbaji makaburi Shakahola

WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kithure Kindiki, ameeleza sababu za kusimamisha utafutaji wa makaburi kutafuta miili ya watu katika msitu wa Shakahola.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kithure Kindiki.

Kindiki alisema jana kuwa kazi ya kutafuta makaburi na kuwafukua waathirika wa  mauaji ya Shakahola imesitishwa.

"Tulisitisha zoezi hilo ili kuruhusu upangaji wa vifaa vya uchunguzi wa maiti 123 za ziada zilizopatikana katika awamu ya pili ya uchimbaji," alisema.

Pia alisema awamu ya pili ya uchunguzi wa maiti itaanza Jumatano ijayo. Uchunguzi wa maiti utafanywa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi.

Hata hivyo, alisema shughuli ya kuwatafuta na kuwaokoa manusura ndani ya Msitu wa Shakahola na shamba la Chakama, itaendelea bila kukatizwa.

"Pia itapanuliwa katika kingo za Hifadhi ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki katika siku zijazo kwa kutumia utafutaji wa ardhini na ndege zisizo na rubani," alisemaght: Getty

Alisema upekuzi na uchimbaji wa makaburi hayo utaendelea tena baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ya uchunguzi wa maiti. BBC