Watu kadhaa wauawa Haiti baada ya gereza kuu kuvamiwa

04Mar 2024
Haiti
Nipashe
Watu kadhaa wauawa Haiti baada ya gereza kuu kuvamiwa

WATU kadhaa wameripotiwa kuuawa nchini Haiti baada ya wanachama wa magenge ya uhalifu kulishambulia gereza kuu kwenye mji mkuu wa taifa hilo Port-au-Prince.

Mamia ya wafungwa pia wametoroka kutoka jela hiyo katika mwendelezo wa wimbi kubwa la machafuko linaloukumba mji mkuu wa taifa hilo la kanda ya Karibia.Inaarifiwa watu watano wameuwawa kwenye mkasa huo wa siku ya Jumapili, ambapo miili mitatu ya watu waliouwawa kwa kupigwa risasi imeonekana kwenye lango la kuingia kwenye katika jela hiyo ambalo liliachwa wazi bila kuwepo na maafisa wa ulinzi na miili ya watu wengine wawili imeonekana barabarani.Hayo yametokea wakati Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry anafanya ziara nje ya nchi akijaribu kunusuru ahadi ya kutumwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kwenda kusaidia kurejesha usalama kwenye taifa lake.