Watoto hao ni wakazi wa Makole, mkoani Dodoma.
Bingwa wa Magonjwa ya Dharura hospitali hiyo, Dk. Asha Iyulla amesema wameanza kuwafanyia vipimo vya awali ikiwamo kuwapima uzito.
Amesema wamebaini mtotonwa miaka saba ana uzito wa kilo 76 na mwenye miaka mitano ana kilo 62.
“Vipimo hivi tulivyofanywa leo ni vya awali. Kesho watafanyiwa vipimo vya ziada, ikiwamo kupimwa wingi wa mafuta kwenye damu katika kliniki yetu ya uchunguzi na matibabu.
"Pia uchunguzi wa vipimo vingine ili kubaini tatizo linalowakabili,” ameongeza Dk. Asha.
Mama mzazi wa watoto hao, Vumilia Elisha, amesema amefurahishwa na mapokezi katika hospitali hiyo na kufarijika, akitumaini watoto wake kupona maradhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Mohamed Janabi, alitoa wito kwa Watoto hao kufika hospitalini na kuwa tayari kutoa huduma za uchunguzi na matibabu kwa watoto hao.
Awali, mama yao alionekana akiomba msaada kupitia video na picha, iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.










