Mwinyikondo amesema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa ya Mtendaji wa Kata ya Talawanda Tumaini Magoso ambaye hakai kwenye eneo la kazi huku utendaji wake ukiwa unasuasua.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Chalinze Mwenyekiti huyo amesema amepokea malalamiko ya Mtendaji huyo lakini pamoja na kuzungumza nae hakuonyesha mabadiliko.
" Kila mtu anatakiwa kusimamia katika nafasi yake na kufanya majukumu yake inavyotakiwa badala ya kila jambo kuelemeakwa Mkurugenzi,".
"Mkurugenzi shughulikia suala la mtendaji wa Talawanda aondolewe malalamiko yamekuwa ni mengi na habariliki kama hawezi kazi kwenye kata mchukue ukae nae hapa ofisini kwako, anaishi Msata eneo la kazi ni Talawanda kwa utaratibu huu hawezi kutimiza vizuri majukumu yake," amesisitiza.
Diwani wa Talawanda Ramadhani Biga amesema mtendaji huyo amekuwa mtoro kwa kutofika kazini kwenye baadhi ya siku za kazi bila kutoa taarifa jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa wananchi kwa kukosa huduma.
Katika Baraza hilo ambalo liliambatana na uwasilishaji wa taarifa za kata viliainishwa vikwazo vingi ikiwemo kwenye Sekta ya elimu na miundombinu ya barabara.
Diwani wa Talawanda Mussa Gama aliomba kufanyika ukarabati wa barabara ambazo zimekuwa vikwazo hususani kipindi cha mvua ambapo baadhi ya maeneo wanafunzi wamekuwa wakikwama kwenda shule.









