Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Godwin Kabalika akizungumza wakati wa kikao cha kutambulisha mradi huo kilichofanyika mjini Singida na kuwashirikisha, amesema wananchi wengine 15,000 watafanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho na 15,000 watapewa miwani ya macho.
Naye Mratibu wa Mradi wa Macho Yangu Mkoa wa Singida, Upendo Minja, amesema kwa mkoa huu wananchi 50,000 watafanyiwa uchunguzi wa huduma za macho, 5,000 watafanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho na wengine 5,000 watapewa miwani katika kipindi cha miaka minne ya utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Singida, Upendo Mwakabalile amesema mradi wa Boresha Macho ambao umekwisha umekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za macho kwa wananchi ulijiwekea lengo la kuwafanyia upasuaji wa mtoto wa jicho watu 5,625 lakini hadi mwisho wa mradi wamefanyiwa watu 7,995 na hivyo kuvuka lengo lililokuwa limewekwa.









