Buswelu ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananfunzi katika shule ya sekondari Kabungu ambapo amemtaka Mkurugenzi na timu yake kutumia jeshi la akiba kuwatafuta wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni.
Mkuu wa shule ya sekondari Kabungu, Abdalah Kombo amesema wamepangiwa wanafunzi 231 na mpaka sasa ni wanafunzi 30 ambao wameripoti.

Aidha, Buswelu amesema hakuna mwanafunzi anaetakiwa kuripoti akiwa na dawati pamoja na mifuko mitano ya simenti kama inavyodaiwa.










