Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mratibu wa Elimu Bora mkaoni Simiyu, Ester Malwa amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia walimu hao kushirikiana na jamii kuweza kuhamasisha mahudhurio ya wanafunzi mashuleni.
Malwa ameongeza kusema kuwa hadi sasa Mkoa wa Simiyu unazaidi ya wanafunzi wenye mahitaji maaluma 605 huku kukiwa na mwitikio toka kwa wazazi wakuwaandikisha watoto wenye mahitaji Maalumu mashuleni.
"Kwa sasa tunaona kunamwitikio wa wazazi wa kuwaandikisha watoto wenye mahitaji maaluma mashuleni tofauti na hapo awali watoto wenye mahitaji maaluma walifungiwa ndani nakukosa fursa yakijiendekeza kielimu"amesema Malwa.










