Wakazi hao walianza kupiga mayowe baada ya Mkuu wa Mkoa huyo kuanza kuruhusu kupokea kero kutoka kwa wakazi hao.
Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwajina la Gondoli Hes aliwakilisha kero hiyo huku wakazi hao wakimsaidia kwa mayowe mazito na uchungu kuashiria wana uhitaji wa huduma hiyo.
Amesema na kumuomba Mkuu huyo wawasaidie wapatiwe eneo ili wajengewe shule kwani wanateseka kwa kipindi kirefu watoto wanaenda umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Wakazi hao waliamua kufunguka kwa kumwambia Mkuu wa mkoa kuwa NSSF wana eneo kubwa kupitiliza ambalo limekaa bila kuendelezwa hivyo waliomba wamegewe eneo hilo wajengewe shule.
Mbali na hilo wakazi hao pia waliomba watengewe eneo la kuzikia ambalo wana uhitaji wa huduma hiyo na huduma zingine za kijamii.
Mwenyekiti wa Mtaa Kata ya Kinondo Mjimpya amesema tayari walishaambiwa fedha Shilingi Milion kumi ilishaingizwa kuanza ujenzi huo lakini bado ujenzi huo haujaanza na hawajui unaanza lini.
RC Chalamila alipomtaka Meneja wa NSSF Kinondoni, Large Materu awajibu wakazi hao amesema wamepokea kilio hicho cha wakazi hao atamfikishia Mkurugenzi Mkuu suala hilo na majibu yatapatikana.
Aidha amesema walishatenga heka nne kwa ajili ya kujengwa shule.










