Vijana watakiwa kujitokeza kuomba nafasi za uongozi

10Apr 2022
Anjela Mhando
Dar es Salaam
Nipashe
Vijana watakiwa kujitokeza kuomba nafasi za uongozi

Katibu idara ya Uhamasishaji na Chipukizi (UVCCM  Taifa  Victoria Mwanziva amesema Chama cha Mapinduzi (CCM)  kinaheshimika na kufahamika kwa mfumo wake wa demokrasia iliyoshamiri ndani yake -

Katibu idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Victoria Mwanziva

- kwa miaka mingi tangu kuanzishwa  baada ya kuungana kwa vyama viwili vikubwa vya siasa nchini ASP kwa Zanzibar na TANU kwa Tanzania bara 1977.

Katibu huyo ameyasema hayo alipozungumza na Nipashe Digital kuhusu vijana na Uchaguzi ndani ya CCM Pamoja na UVCCM ambapo amesema  vijana wamekuwa ni nguzo imara ya kushamirisha demokrasia kwa kuaminika kuwa tanuru mahususi la kuoka na kuzalisha viongozi katika njanja mbalimbali za uongozi ndani ya Chama lakini pia Serikalini.

Kwa mujibu wa katibu hiyo amesema kuna msemo usemeao usipoongoza basi utaongozwa Muda umefika, kipyenga kimeshapulizwa, zoezi la kuchukua fomu maeneo yote nchini linaendele ni wakati wetu vijana kuchangamkia fursa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zilizoanishwa kwa mujibu wa katiba ya CCM na Kanuni za umoja wa Vijana wa (UVCCM).

Ameongeza kuwa Vijana hatupaswi kubaki nyuma na kubweteka ni wakati sahihi kwetu vijana kujitokeza kwa wingi, kuchukua, kujaza, na kurejesha fomu za uongozi ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa , kuonyesha vipaji na uwezo wa uongozi uliopo ndani ya Vijana huku tukisimamia kauli mbiu ya uchaguzi isemayo ‘Chama Imara Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu’.

Aidha  amesema  kuwa Mwenyekiti  wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati anaongea na vijana Jijini Mwanza  June 15 2021  alisema “Vijana ni engine ya maendeleo kwa taifa lolote lile na taifa lolote ulimwenguni haliwezi kuendelea bila kuwatumia vijana wake”.

Hii inatuamsha vijana na kuiona thamni yetu katika Taifa letu la Tanzania kwa kuona ni jinsi gani mwenyekiti wa chama chetu anatambua umuhimu wa uwepo wa vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na hata nje ya Chama kwa maendeleo ya Taifa letu.

Nafasi za kugombea uongozi ndani ya UVCCM ni nafasi za vijana kwa mujibu wa katiba ya CCM na kanuni za UVCCM, hivyo ni jukumu letu vijana kujitokeza na kugombea nafasi zote za uongozi zilizoanishwa kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa.

Zipo nafasi nyingi za kugombea uongozi ndani ya UVCCM kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa hivyo nawasihi sana vijana wote nchini waliotimiza vigezo na kujipima kwa uwezo wao kujitokeza kwa wingi kugombe nafasi zote ndani ya umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwani hakuna mtu yoyote nje ya vijana anayeweza kuchukua nafasi hizo kama nilivyoeleza awali kuwa upekee wa nafasi za uongozi ndani ya UVCCM ni nafasi za vijana pekee tofauti na ndani ya CCM, UWT na Jumuiya ya Wazazi ambapo nafasi za uongozi huko ni kwa mwanachaa yoyote aliyekizi vigezo vya kikatiba na kikanuni ana haki ya kugombea nafasi hizo.

Hata hivyo aliwataka vijana kuwa waadilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuichafua taswira halisi ya uchaguzi ndani ya UVCCM, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM kwenye chaguzi zake tangu kuanzishwa kwake kwani  imekua ni mfano wa kuigwa kwa kupinga vitendo ya kubebana, Rushwa, na kujuana  hali inayopelekea kupatikana kwa viongozi makini, na hodari ambao wanabeba maono na mahitaji halisi ya vijana katika Taifa letu. 

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Raisi Samia Suluhu Hassan katika kilelele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Januari 07, 2022 alitausa vijana kuwa makini katika chaguzi mbalimbali kwa kusema “ Vijana msitumike kukipasua Chama nendeni kakiimarisheni Chama na Jumuiya yenu, vijana msitumike vibaya”. Lakini pia akaenda mbali kwa kusema “ Uzoefu unaonyesha kuwa vijana mnageuzwa ngazi na kuwabeba watu wanaotaka uongozi kwa tama za fedha na ahadi za uongozi, mjiulize kama hao mliowabeba wangeonyesha utendaji mzuri leo hii msingekua na changamoto mnazozisema”.

Kwa kauli hizi za Mwenyekiti wetu na Rais Samia Suluhu Hassan zinatuamsha vijana kuongeza umakini kwenye mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ndani ya CCM na Jumuiya yetu ya Umoja wa Vijana wa CCM kwa kuhakikisha hatushiriki katika vitendo vyovyote vile vya kuwabeba wagombea wala kutoa au kupokea rushwa kwa kigezo cha kumpigia kura au kumnadi mgombea flani na hapo ndipo tutakua tumishi kwenye kauli mbiu ya uchaguzi mkuu ndani CCM ya mwaka 2022 ‘Chama Imara, Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu’. Amesema Katibu huyo.