Wakili wa serikali Happyness Mwakanyamale amesema kuwa hayo leo katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam wakati kesi hiyo, ilipotajwa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ushindi Swalo, wakili huyo amesema kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa ambapo ilipangwa Februari 19 mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Mrisho ambaye ni mkazi wa Boko, Tegeta, anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 31 mwaka 2023 eneo la Boko Magengeni.
Ilidaiwa kuwa, akiwa eneo hilo alikamatwa akisafirisha dawa za kulevya ,Cocaine gramu 326.46.










