Viongozi hao wametoa kauli hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Thomas Apson, katika kikao cha kuhamasisha sensa na kuchanja chanjo ya corona kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Mashehe, Wachungaji, Malaigwanani pamoja na Mangi wa kabila la Kichaga wa Wilaya hiyo.
Akizungumza Shehe wa Wilaya hiyo Abubakari Hashimu, amesema zoezi la sensa tumeliunga mkono kuanzia itangazwe na mimi kama Shehe wa Wilaya tumetangaza kwenye misikiti yetu hata sasa hivi nimetoka kwenye majukumu hayo ya kuhamasisha nilikuwa na kikao na zaidi ya watu 50 kwenye Wilaya yetu.
"Sensa ni sehemu ambayo serikali inataka iwatambue wananchi wote ili hata serikali ikiagiza dawa itambue inaagiza dawa za watu wangapi, serikali ikitaka kuleta maji ijuwe inaletea maji wananchi wangapi hivyo tumeipokea kwa mikono miwili na tutaitangaza na tutahesabiwa na watu wetu wote" amesema Shehe Hashimu
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mila wa kabila la kifugaji Maasai (Laigwanani) wa Afrika Mashariki Joseph Laizer, amesema yupo tayari kuhesabiwa pamoja na wananchi wa Jamii hiyo kwani tayari ameihamasisha kushiriki sensa na imekubali kuhesabiwa lakini bado ataendelea kuhamasisha ili serikali iweze kuwapatia huduma kulingana na idadi yao .

Naye kiongozi wa Mila wa kabila la Kichaga wilayani hapo Mangi Kileo, amesema kabla ya kikao hiki nimeshakaa na wenyeviti wote wa ukoo, makatibu wao, wenyeviti wa Jumuiya za koo, wenyeviti wa Jumuiya za wanawake na vijana pamoja na waweka hadhina wao ambapo amewaita kwenye kikao kwa ajili ya kuhamasisha sensa na wamepokea kwa mkono mmoja rai ya kuhesabiwa na kuendelea kuhamasisha wana ukoo wao wote kushiriki zoezi la Sensa Agost 23.
Kuhusu Kuchanja chanjo ya corona Laigwanani wa Afrika Mashariki Joseph Laizer, amesema tayari ameshachanja chanjo hiyo na ataendelea kuhamasisha Jamii hiyo kuchanja kwa wingi ili kutengeneza kinga imara kwa jamii hiyo, huku Shehe wa Wilaya hiyo akisema ataendelea kuhamasisha waumini katika kuchanja kwa wingi ili kutokomeza ugonjwa wa corona unaotesa Taifa.










