Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa hiyo, Octavian Mshiu wakati wajumbe wa bodi hiyo walipotembelea na kukagua barabara ya Shule ya Msingi Igoma yenye urefu wa mita 370 inayojengwa kwa mawe ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 70 pamoja na barabara ya Nyashana ambayo tayari imeshakamilika.
Ameeleza ujenzi wa barabara za mawe zinadumu muda mrefu hivyo kuokoa gharama za matengenezo tofauti na kutegemea lami ambayo inaagizwa nje ya nchi.
"Natoa wito siyo Mwanza tu kila mkoa ambao unaweza kujenga barabara na madaraja kwa teknolojia mbadala wafanye hivyo kwani itakuwa imeisaidia serikali kuokoa fedha nyingi."amesema Octavian
Meneja TARURA Mkoa wa Mwanza, Gudluck Mbanga,ameeleza kuwa ujenzi wa barabara za mawe mkoani Mwanza umeokoa fedha nyingi ambazo serikali imekuwa ikitumia katika kurudia matengenezo katika barabara za gravu pamoja na kutoa ajira kwa wazawa.
Ameeleza Jiji la Mwanza kwa maana ya Wilaya ya Nyamagana na Ilemela wana zaidi ya Km 2000 za barabara huku za mawe ni km 16 pia tatizo lililopo kwenye jijini ilo lenye miinuko yenye mawe vipindi vya mvua muunganiko wa mawe na gravu unakuwa siyo mzuri na kuchangia magari kushindwa kuhimili kupanda."Asilimia kubwa ya barabara zetu ni udongo tunahitaji sana barabara za mawe kwa kiasi kikubwa tulichofanya ni kama tuna sawa na asilimia 0.2, tunashukuru pamoja na vyanzo vya fedha kwa kumalizia barabara hizi ambazo nyingine zipo katika hali siyo nzuri,"ameeleza Mbanga.
Naye Mhandisi wa barabara Wilaya ya Nyamagana Jane Mdula, ameeleza kuwa gharama za ujenzi wa barabara za mawe ni nafuu kidogo ukilinganisha na nyingine akitolea mfano barabara hiyo ambayo ina urefu wa mita 370 na gharama yake ni milioni 167 pia utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mawe kwa asilimia kubwa inafanywa na watu na siyo mitambo.
"Hapa tunatengeneza ajira kwa watu wanaochonga mawe ya kujenga barabara ambayo yanachongwa kwa mkono pia ujenzi wake ni wa gharama nafuu ukilinganisha na ujenzi wa barabara nyingine,"ameeleza.
Ireni Mussa ni mmoja wa wafanyakazi katika mgodi wa mawe yanayotumika katika ujenzi wa barabara hizo wameshukuru serikali kutekeleza miradi ya barabara za mawe kwani zimewasaidia kuinua uchumi wao.
"Wakati nakuja Mwanza kutokea Musoma nilikuwa na wakati mgumu kwa sababu sikuwa na ramani lakini kupitia shughuli hii ya kuchonga mawe imenisaidia,"ameeleza Irene Musa.
Naye Monica Mawi,ameeleza kuwa kupitia kazi ya kuchonga mawe ameweza kuwapeleka watoto shule pamoja na kurekebisha nyumba yake.
Hata hivyo Ibrahim Musa,ameeleza kuwa kupitia shughuli ya uchingaji wa mawe yanayotumika katika ujenzi wa barabara zimemsaidia kujiingizia kipato ambacho usaidia wazazi wake.










