Hatua hiyo inafuatia kuanzishwa kwa huduma ya usafiri wa mabasi ya haraka (DART) katika barabara ya Morogoro inayoanzia Mbezi Luis kupitia Kimara mwisho.Mabasi hayo ya DART yanaanzia Kimara kuelekea Morocco, Kariakoo, Kivukoni na kurudi kwa kutumia njia hizo.
Ruti hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia kesho ambapo nia tatu za daladala za kuanzia Mbezi kwenda Kariakoo, Kimara Muhimbili, Simu 2000 kwenda Posta na Kivukoni zimefutwa kabisa.
Njia mpya za daladala zilizotajwa ni kutoka Mabibo kwenda Kariakoo ambapo daladala zitapitia barabara za Kigogo, Kawawa, Uhuru, Shauri Moyo, Lindi hadi kituo cha DART cha Gerezani.
Mabasi yatakayotoka Mabibo kwenda Muhimbili yatapitia Kigogo, Jangwani, Twiga, Swahili, Umoja wa Mataifa hadi Muhimbili.
Taarifa hiyo ilisema mabasi ya kutoka Mabibo kwenda Posta Mpya yatapitia Kigogo, Kawawa, Uhuru, Bibi titi, Maktaba hadi Posta Mpya, wakati yale yanayotoka Mabibo kwenda Makumbusho yatapitia Mabibo, Morogoro, Shekilango, Tandale Uzuri, Kawawa, Mwinyijuma hadi Makumbusho.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabasi yatakayotoka Makumbusho kwenda Kariakoo ndiyo yaliyobadili njia zaidi baada ya kupangwa kupita New Bagamoyo Road, Shekilango, Morogoro, Mabibo, Kigogo, Kawawa, Uhuru, Shauri Moyo, Lindi hadi kituo cha DART cha Gerezani.
Taarifa ya Sumatra ilisema mabasi yatakayotoka Makumbusho kwenda Posta Mpya yataendelea kupita New Bagamoyo, Ali Hassan Mwinyi, Bibi Titi, Maktaba hadi Posta Mpya.
Ilisema mabasi yanayotoka Makumbusho kwenda Muhimbili yatapita New Bagamoyo, Ali Hassan Mwinyi, Umoja wa Mataifa, Maliki hadi Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, daladala zinazotoka Tegeta, Bunju, Kunduchi na Kawe kuelekea kituo cha DART cha Moroko yatapita Old Bagamoyo, New Bagamoyo, Kawawa hadi kituo cha DART cha Moroko.
Sumatra ilisema daladala zinazotoka Tegeta, Bunju, Kunduchi na Kawe kuelekea Kituo cha DART cha Mwinjuma zitapitia Old Bagamoyo, New Bagamoyo, Malanga, Mwinjuma hadi kituo cha DART cha Mwinjuma.
Ilisema daladala za kutoka Mbagala, Temeke na Tandika kwenda Muhimbili zitapita barabara ya Kilwa, Bandari, Nyerere, Bibi Titi, Ali Hassan Mwinyi, Umoja wa Mataifa, Maliki hadi Muhimbili.
Daladala za kutoka Gongolamboto, Ukongam, Banana kwenda Muhimbili zitapita barabara za Nyerere, Bibi Titi, Ali Hassan Mwinyi, Umoja wa Mataifa, Maliki hadi Muhimbili, taarifa hiyo ilisema.
Sumatra iliwakumbusha wamiliki wa daladala, wakiwemo madereva na wafanyakazi wao kuzingatia masharti ya leseni zao kwa kutoa huduma katika njia walizoruhusiwa.










