...msingi na sekondari zilizojengwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi (BOOST) na Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Singida baada ya kuzindua Shule ya Msingi Imbele na shule ya Sekondari Mwanamwema zilizopo mkoani Singida kwa niaba ya shule mpya 302 zilizojengwa nchi nzima kupitia BOOST na SEQUIP ametaka shule hizo zitunze ili ziendelee kuwanufaisha watoto watakaokuwa wakisoma kwenye shule hizo ambazo serikali imetoa Sh.bilioni 230 kuzijenga.
Naye Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amesema katika kipindi cha kuanzia 2005 hadi 2026 serikali imetenga Sh.Trilioni 1.15 kwa ajili ujenzi wa shule za awali,msingi na sekondari kupitia miradi ya BOOST na SEQUIP.
Alisema hadi sasa zimekwisha kutolewa Sh.bilioni 230 ambazo zitatumika kujenga shule za msingi 302,shule za awali 364 na madarasa 2929 na kwamba hadi kufikia Septemba mwkaa huu shule mpya 194 zimejengwa,shule za awali 294 zimejengwa na madarasa 2303.










