Nsimbo yajipanga kuanza biashara ya hewa ukaa

22Dec 2023
Neema Hussein
Nsimbo
Nipashe
Nsimbo yajipanga kuanza biashara ya hewa ukaa

Wakuu wa idara mbalimbali na viongozi wa vijiji katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, wameshauriwa  kulinda misitu kwa kiasi kikubwa ili waweze kufanikisha uanzishwaji wa biashara ya hewa ukaa katika halmashauri hiyo.

 

Ushauri huo umetolewa na Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Bruno Nicolaus  katika ziara iliyofanywa na viongozi hao kwalengo la kujifunza biashara ya hewa ukaa katika halmashauri ya Tanganyika.

Frolentina Ilumba Afisa Misitu Halmashauri ya Nsimbo amesema halmashauri tayari inafursa ya kuanza biashara ya hewa ukaa kwa vijiji vitatu ambavyo tayari vimefanyiwa matumizi bora ya ardhi kwa kutenga misitu kwaajili ya kuanza kunufaika na biashara hiyo.

Rafael Kalinga, ni diwani wa Machimboni na Elieza Samweli Diwani wa Mtapenda ni miongoni mwa washiriki wa ziara hiyo ambapo wamesema kupitia biashara hiyo vijiji vilivyozungukwa na misitu hiyo pamoja na halmashauri vitanufaika hivyo watahakikisha wanasimamia misitu isiharibiwe.