Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake kwa ngazi ya halmashauri yaliyofanyika kata ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Katavi Judith Mbukwa amesema asilimia kubwa ya watu wa Katavi hufungia wagonjwa ndani na kuanza kuwatibu kwa kutumia dawa za kienyeji kwakuhisi wamelogwa.
Amesema serikali inaendelea kujenga hospitali,vituo vya afya na zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi hivyo anashangaza na wananchi kutotumia vituo hivyo nakuendeleza mambo ya zamani ya kutibiana wenyewe ndani.
Lucy kagine ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya katumba wakati akisoma taarifa kwa mgeni rasimi amesema
hali ya ubaguzi katika ugawaji wa rasilimali fedha kwa wanawake imekua ikipewa nafasi ndogo kwa baadhi ya makabila katika halmashauri ya Nsimbo hali hiyo imetajwa kuchochea shughuli haramu zisizokubalika katika jamii kamavile ukahaba kwa watoto wa kike nakusabisha kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi, wimbi la watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Maadhimisho hayo yalienda sambamba na kufanya matendo ya huruma ambapo msaada wa vitu mbalimbali ulitolewa kwa watu wenye u
hitaji.









