NEC yateua Madiwani watano Viti Maalum kujaza nafasi za waliofariki

01Feb 2024
Na Mwandishi Wetu
DODOMA
Nipashe
NEC yateua Madiwani watano Viti Maalum kujaza nafasi za waliofariki

Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha Januari 29,2024, imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum watano (5) kujaza nafasi zilizokuwa  wazi katika Halmashauri tano (5) za Tanzania Bara. 

Uteuzi huo umezingatia matakwa ya kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura 292.

Uteuzi wa Madiwani hao wanawake wa viti maalumu umefanyika baada ya Tume kupokea barua kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, aliitarifu Tume juu ya uwepo wa nafasi wazi za madiwani wanawake wa viti maalum katika Halmashauri tano (5) za Tanzania Bara. Nafasi hizo zimetokana na vifo vya Madiwani hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tume baada ya kupokea taarifa hiyo ilimfahamisha Katibu Mkuu wa CCM juu ya uwepo wa nafasi wazi. 

Chama hicho kiliwasilisha majina ya wanachama waliopendekezwa kuteuliwa kuwa madiwani wanawake wa viti maalum ambao ni Mecha Gudluck Matile, Joyce Milembe Aenda, Sharifa Hassan Magalagala, Clementina Daudi Mateja na Mariam Abdi Galu.