Waziri Nchemba ameyasema hayo jana jioni wakati akitolea ufafanuzi wa maswali yaliyotolewa na wananchi katika mkutano wa ziara ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda uliofanyika mkoani Singida.Wananchi hao walieleza mikopo ya kausha damu inawatesa hawaishi kwa raha kwa kuwa wananyang'anywa mali zao na wengine ndoa kuvunjika.Amesema wananchi wasisite kutoa taarifa katika ofisi za mikoa na wilaya ili serikali iwachukulie hatua ikiwemo kuwafutia leseni zao.Awali Makonda alitaka kupata ufafanuzi kwa Waziri Nchemba kwa kuwa kero hiyo waliyoielewa wananchi inawatesa wengi huku akitaka apatiwe majibu kutokana na maswali yake matatu. "Mheshimiwa Waziri na Mimi katika hiyo mikopo ya kausha damu npina maswali 10 ila hapa nitauliza maswali matatu je kausha damu wana leseni?, Na kama wanazo anayepiga mahesabu ya riba ni nani? na kwenye riba yao serikali inanufaika vipi?," alihoji Makonda.Amesema ni kweli serikali imetoka leseni na riba wameweka kwa utaratibu wao si wizara wala Waziri anayepata chochote. Waziri amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kuondoa usumbufu wanaopata wananchi kwa kumuelekeza Gavana wa Benki Kuu (BoT) na idara ya mikopo ndani ya Wizara ya fedha kupitia upya masharti ya vibali kwa leseni hizo na kuweka upya utaratibu mzuri.Amesema kinachofanyika kwa sasa ni kupitia upya leseni hizo na kuweka utaratibu mzuri ili kuepuka na mikopa ya kausha damu.Waziri amesema tayari Serikali imeshafuta leseni holela kwasababu ya uwekaji wa masharti ya riba kubwa na kuwanyanyasa wananchi."Hizo kausha damu zina maabusu zao wanawachukua watu na kuwaweka humo hii sio jambo nzuri wananchi tupatieni taarifa ya hao wanatoa mikopo kwa riba kubwa tuwafutie leseni zao," amesema Waziri.










