Mwanajeshi aua wanajeshi wenzake kwa risasi

22Jan 2024
Iran
Nipashe
Mwanajeshi aua wanajeshi wenzake kwa risasi

MWANAJESHI mmoja amewashambulia kwa risasi na kuwauwa wanajeshi wenzake watano katika hospitali inayohudumia wanajeshi nchini Iran.

Shirika la habari la serikali ya Iran, IRNA limeripoti kuwa, tukio hilo limetokea jana katika Wilaya ya Kerman, likimnukuu brigedia jenerali katika wilaya hiyo.

Kulingana na ripoti, mwanajeshi huyo aliingia katika hospitali inayohudumia wanajeshi na kuanza kufyatua risasi kiholela. Haikubanika mara moja alikuwa na lengo gani lakini alifanikiwa kutoroka.

Matukio kama hayo ni nadra sana kutokea nchini humo. Hivi karibuni, washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijilipua na kuwaua karibu watu 100 katika wilaya hiyo.

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu lilidai kuhusika na shambulio hilo.