Akizungumza jana kwa njia ya simu, Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Jumamosi iliyopita.
Sabas alisema Jennifer alijifungua Januari 29, mwaka huu, katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
"Lakini bahati mbaya mtoto wake hakutimiza miezi yaani njiti na kesho yake asubuhi aliamka na kunyonyesha mtoto kisha alipotea," alisema.
Alisema baada ya wauguzi kuona muda umepita bila kumwona, walianza kumtafuta na kesho yake walumkuta juu ya mti akiwa amejinyonga.
Sabas alisema baada ya kugundua tatizo hilo wauguzi walitoa taarifa polisi na kuuhifadhi mwili huo chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa Sabas, baadaye ndugu zake walipewa taarifa na kukabidhiwa mwili kwa ajili ya taratibu za mazishi.










