Hayo yameelezwa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wakati wakijadili rasimu ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2024/25.
Wamesema kutokamilishwa kwa vyumba 57 vya madarasa ya shule za msingi vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi hadi kwenye lenta tangu mwaka juzi ni kuwakatisha tamaa wananchi kuchangia miradi ya maendeleo.
Akijibu malalamiko ya madiwani hao, Kaimu Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wilayani humo, Hauson Revelian, amewataka kuwa na subra kwani tayari halmashauri hiyo imeomba fedha kutoka serikali kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma hayo zikiwemo nyumba 6 za watumishi.
Pia amesema hali hiyo isiwakatishe tamaa badala yake waendelee kuwahamasisha wananchi kuibua miradi kwaajili ya maendeleo ya umma na pale fedha zinapopatikana Halmashauri inamaliza sehemu yake.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Leo Rushahu, amesisitiza ushirikiano katika ukusanyaji mapato ya ndani kwa madai ndiyo mwarobaini wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kupitisha kwa kauli moja makisio ya bajeti ya shilingi bilioni 48.3 itakayotekeleza.










