na hivyo kuondokana na kero ya kutembea umbali mrefu wa kilometa 70 kwenda kusoma katika Sekondari nyingine iliyopo kata ya Rungwa.
Ametoa agizo hilo jana (Julai 29, 2023) akiwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa baada ya kutembelea shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa kusaidiwa na halmashauri na wadau mbalimbali lakini tangu mwaka 2019 utekelezaji wa kuijenga ulipoanza haijaanza kutumika na hivyo wanafunzi wanaofaulu kutoka kata ya Mwamagembe wanapelekwa kata ya Rungwa ambako ndiko kuna Sekondari.
Mlata alisema bado hakuna jitihada za madhubuti zilizochukuliwa kuhakikisha ukanda wa kata ya Mwamagembe na Rungwa ambazo zinapakana na Mkoa wa Mbeya watoto wanapata elimu na hivyo wanafunzi wanaotoka kata ya Mwamagembe wanapokwenda kusoma Kata ya Rungwa kutokana na umbali watoto wa kike wanaishia kuwa wake za watu au kufanya kazi kwenye nyumba za watu.
Naye Diwani wa Kata ya Mwamagembe, Jonathan Dulle, kutokana na kukosekana kwa Sekondari katika kata hiyo wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na Sekondari kutokana na umbali mrefu wa kwenda kusoma Kata ya Rungwa wengi wamekuwa hawaendi shule na kutoa mfano mwaka jana kati ya wanafunzi 96 waliohitimu 38 hawakujiunga na Sekondari hadi sasa na hawajulikani walipo.










