-na serikali wilayani hapo kutumia nafasi hizo kuwasema viongozi wa CCM na kukisema Chama vibaya.
Meijo ametoa kauli hiyo jana katika maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi, sherehe zilizoadhimishwa na jumuiya ya wazazi ambapo kimkoa zimefanyika wilayani Siha katika ukumbi wa Roman Catholic (RC) .
Kwa mujibu wa Meijo amesema Chama hicho kimeanzishwa kwa malengo mahususi ya kuwasaidia wana CCM na kuwasaidia wa Tanzania lakini pia Chama hicho kimetoa dhamana ya kuwa viongozi ndani ya Chama na ndani ya Jumuiya ili kuwasaidia wana Chama na kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Siha.
"Ninataka niseme mimi ni Mwenyekiti wa wazazi Wilaya ya Siha na hili nasema mbele ya viongozi na wana CCM na wanajumuiya kuna haja ya kukiheshimu Chama chetu kwani kumdhalilisha mwana CCM na viongozi ni aibu kubwa na nifedheha lakini Chama hiki hatuwezi kukubali kamwe" amesema Meijo
Aidha amesema hawawezi kukubali kamwe ikiwezekana Leo kupeleka habari hizi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aweze kufanya kufanya maamuzi magumu juu ya wale viongozi ambao wamepewa dhamana ndani ya Chama lakini wamepewa dhamana ndani ya Serikali kukisemea Chama hiki vibaya na kuwasema viongozi wanaotokana na Chama hiki ambao wanafanya kazi kubwa ndani ya Wilaya ya Siha.
Wilaya ya Siha Imefanya kazia kubwa pamoja na viongozi wa Wilaya wamefanya kazi kubwa ya maendeleo lakini sisi tuliopewa dhamana tunakosea jambo moja kuwasema viongozi hadharani wakati tuna vikao ,tuna nafasi ya kusemea ndani ya vikao ,nimumuombe mwenekiti wa CCM wilaya zipo kamati za maadili ndani ya Wilaya, zipo kamati za maadili za mkoa, zipo kamati za maadili ngazi ya Taifa .










