RC Makalla ametoa onyo hilo wakati wa zoezi la usafi wa pamoja Soko la Machinga Complex ambapo amewaelekeza viongozi wa masoko yote kudhibiti na kusimamia agizo hilo.
Aidha RC Makalla ametumia zoezi hilo kuwahakikishia wafanyabiashara waliokuwa Soko la Kariakoo kuwa ujenzi ukikamilika kipaumbele kitakuwa kwa wale waliokuwepo awali.
Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kupiga marufuku ufanyaji biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa na kuwataka kwenda kwenye masoko rasmi ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali hususani mikopo.










