Kilio Cha wafugaji hao kimewasilishwa katika Baraza la Madiwani Nsimbo baada ya kupokea malalamiko ya wafugaji kukosa maeneo ya malisho na kupelekea kupigwa faini pindi wanapoingiza mifugo yao kwenye maeneo ambayo yamehifadhiwa.
Ombi hilo limepatiwa majibu na Afisa Kilimo Halmashauri ya Nsimbo, Daniel Walakunga, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed Ramadan pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambapo wamesema hawana uhakika kama serikali kuu inaweza kukubali ombi hilo sababu tayari ilisha mega eneo kutoka kwenye hifadhi na likarudishwa kwa wananchi.
Aidha baraza hilo limesisitiza maadhimio yote yanayotolewa na baraza yatekelezwe ipavyo ili kuepusha migogoro na kujirudia kwa hoja katika vikao vingine vya baraza.










