Wamepitisha ombi hilo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 14 ambapo wamwsema wamejipima vigezo vinavyostahili kupandishwa hadhi kuwa Manispaa na kubaini kuwa wanakidhi ikiwemo idadi ya wananchi ambao kwa sasa wako zaidi ya laki tano.
Wamesema Halmashauri hiyo Ina vigezo vya kuwa Manispaa, ikiwemo idadi ya watu huku wakielwza kwamba wakati Halmashauri hiyo inaanzishwa mwaka 2000 kulikuwa na Kata 15 na sasa tuna Kata 25.
Ametaja faida watakazonufaika nazo iwapo ombi hilo litapitushwa na TAMISEMI kuwa ni pamoja na kutengewa bajeti kubwa kutoka Serikalini ambayo itakuwa inawesesha kutekelezà miradi mikubwa itakayotatua vikwazo kwa wananchi
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Waziri Kombo amesema kuwa moja ya vigezo vinavyoweza kuwapa uwezekano wa kupata manispaa ni makusanyo ya mapato ambapo katika robo ya pili ya mwaka 2023/2024 wamekusanya sh.6.5 bilioni kati ya bajeti ya sh 13 bilioni
Kombo ametaja vigezo vingine kuwa ni uwepo wa huduma za kijamii Taasisi zinazotoa huduma za pesa uwepo wa viwanda viwanda na uwezo wa Halmashauri kujitegemea kwa asilimia 25 kwa bajeti.
"Kati ya hizo sh.3.7 tumezipeleka kwenye miradi ya maendeleo lakini hata hivyo mahitaji bado yanahitajika hivyo tukipandishwa hadhi kuwa manispaa tutakuwa tinapewa bajeti ya miradi mikubwa"amesema.
Kwa upande wa barabara amesema kuwa ingawa jukumu hilo liko chini ya mamlaka zingine lakini kwa upande wao wamejenga barabara ya kiwango cha lami km.0.48 kwa gharama ya sh.580 milioni ambayo imekamilika
Diwani wa Tegerea Shabani Manda amesema kuwa endapo ombi hilo litapitushwa litachochea maendeleo ya wananchi.










