Akiwasilisha rasimu ya makisio ya mpango na bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 juzi katika mkutano maalum wa baraza hilo ambao ulijadili mapitio ya utekelezaji wa mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na makadirio ya bajeti kwa mwaka huu. Afisa Mipango, Emmanuel Dyelu, alisema fedha hizo Sh.bilioni 13.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh.bilioni 6.4 kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba,alisema ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo umekuwa mzuri na kufikia karibu asilimia 82 mapato huru ambayo yakichanganywa na mapato lindwa inakuwa takribani asilimi 70.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,John Mgalula, alisema halmashauri imejipanga kutekeleza miradi yote iliyopanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ili kuwaletea maendeleo wananchi.










