Maafisa Ugani Singida apewa mtihani mkali

06Feb 2024
Thobias Mwanakatwe
Singida
Nipashe
Maafisa Ugani Singida apewa mtihani mkali

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amewapa mtihani Maafisa Ugani kwamba wataanza kupimwa utendaji wao wa kazi kwa vigezo vinne ambavyo kama watashindwa kuvitimiza ajira zao zitakuwa rehani.

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba.

Amesema hayo leo wakati wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya hali ya usambazaji wa mbolea na mbegu za alizeti zenye ruzuku ya Serikali katika halmashauri ambacho kiliwashirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Kilimo, wawekezaji wenye viwanda, viongozi wa dini na taasisi mbalimbali za mkoani hapa.

“Niwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri wawe wananipa ripoti ya Maafisa Ugani kila wilaya ambapo tumeweka vigenzo vinne, Mosi, wametembelea wakulima wangapi,pili, matumizi yam bole,je amehamasisha wakulima wangapi kwenye eneo lake, tatu,ugawaji wa mbegu za alizeti na nne je amepima mashamba mangapi afya ya udongo,” amesema.

Serukamba amesema Maafisa Kilimo wanapaswaa kuweka mkazo katika kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kutumia mbolea na mbegu bora kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao ili mkoa huu uweze kuingia katika ramani ya uzalishaji nchini.