Kwa mara ya kwanza taasisi hiyo imeanza na kuwafikia wanafunzi mabinti ambao wamepoteza wazazi wao wote wawili (yatima) waliopo katika Shule ya Sekondari BethSaida Orphan Centre iliyopo MbeziMpigi Magohe jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo Mary Kiria amesema taasisi hiyo imekuja kujikita kutoa elimu kuwajengea uwezo mabinti wadogo waliopo mashueni katika masuala ya uongozi, uchumi na ujasiriamali ili waweze kujiamini na kuwa na utambuzi wa maisha.
Kiria amesema msichana mdogo hasa yatima anapopewa elimu ya utambuzi ya uongozi, uchumi na elimu nyingine zihusuzo ujasiriamali zitamjengea uwezo wa kuendeleza maisha na kujiamini katika nyanja za maisha ikiwemo na kuweza kujiari bila kusubiri ajira kutoka serikali na kwingineko.
Mbali na kutoa elimu hiyo taasisi hiyo ilirudisha hisani kwa jamii kwa kupeleka misaada ya vyakula na taulo za kike katika shule hiyo ya wasichana waishio bila wazazi na kujumuika pamoja kwa kukata keki ya upendo na wanafunzi hao.
Amefafanu kufanya hivyo ikiwa ni katika kurudisha katika jamii na wao wameona waje wawaguse watoto yatima ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Kwani Mungu anasema Dini nzuri ni ile inayorudisha na kuwasaidia wahitaji na sisi tumeona leo tuje tuwaguse wahitaji watoto wetu yatima tufurahi pamoja na tumewaletea kile tulichojaaliwa” amefafanua Kiria
Akizungumza kwa niaba ya walimu shuleni hapo, Mwl. Agness Elfasi amesema shule hiyo ilianza mwaka 2006 ikiwa kama kituo cha kulelea watoto yatima na baadae mkuu wa shule hiyo Holiness Mushi akaanzisha na shule kulingana na uhitaji mkubwa wa wanafunzi hao.
Amesema shule hiyo ya bweni inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kukosa vyakula kwa baadhi ya nyakati pindi kinapoisha wanafunzi wamekuwa wakishinda ama kulala na njaa kwakuwa shule hiyo haina wafadhili ukiachana na mkuu mwenyewe wa shule anayelea watoto hao.
Pia tumekuwa tukikabiliwa na changamoto huduma ya afya pindi watoto wanapojitokeza kuumwa usiku mkubwa huduma hiyo wanaifata nje na mbali na hapo shuleni, hivyo wanaiomba Serikali iwaangalie kwa macho mawili waweze kupata huduma hiyo hapo shuleni.
Glory Cosmas(17) dada mkuu shuleni hapo amesema wanaiomba Serikali iwapatie majengo ya maabara kwani kuna maabara ya somo la Chemistry pekee na wanauhitajiwa maabara ya Biology na Phisics.









