Fereji alieza kuwa kiongozi huyo, alimfuata kwa ajili ya kumuomba awaazime nyumba hiyo ili kuendesha shughuli zao za chama.
Makonda aliagiza kiongozi huyo aliyechukua nyumba ya Fereji kuhakikisha leo anapatiwa nyumba yake.
Makonda alitoa kauli hiyo akiwa na wananchi katika Halmashauri ya jiji la Tanga ambapo aliwataka viongozi hao kufungua ofisi leo na kutoa huduma baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwemo migogoro ya ardhi.
Awali Fereji amesema nyumba yake aliombwa na Meja Mstaafu Mkoba kwa sababu ipo jirani na CCM walimuambia wanataka waweke makatibu wao alikubali kwa sababu yeye ni mwanachama wao.
" Mimi kwa sababu ni mwanachama wa CCM nikasema sawa hakuna shida makatibu ni wetu nikatoa hiyo nyumba yenye ofa ya miaka 21 ambayo alikuwa nayo mmiliki wa kwanza nikauziwa nimekaa nayo miaka 11 mpaka leo hii ofa yangu inaonyesha ni miaka 33," amesema.
"Mwaka jana nikaona wanaanza ujenzi wa tofali katika banda la uwani nikamfuata Mwenyekiti nikamuuliza ni vipi akanijibu hii yetu bwana sio yako tena nikamuambia inakuwaje mimi mwanachama wa CCM hivi kimnyang'anye nyumba mwanachama wake nikamuambia hiki sio chama ni wewe.. chama hakiwezi kufanya hivi, ".
Fereji amesema ilibidi aende ardhi kuhakiki hati yake kujua kama iliibiwa au la akajulishwa namba 62 ni nyumba yake akatakiwa kuonyesha ofa yake na akatakiwa kueleza tatizo.
Makonda baada ya kusikiliza alimuuliza" Aliyekuambia hiyo nyumba sio yako ni nani je yupo hapa Katibu wa Wilaya unamjua aliyemtaja ina maana ni Mwenyekiti wa hii Wilaya ya Tanga? Duuu.. Ndio amechukua hiyo nyumba, " amesema Makonda.
" Katibu una dakika mbili kuongea naye na kumtafutia Mwenyekiti akabidhi nyumba yake leo, " amesema Makonda huku akishangiliwa na wananchi.