Makabidhiano ya gari hilo pamoja na vitanda vya wagonjwa yamefanyika leo Februari 9, 2024, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,Chama pamoja na Wananchi.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi gari hilo na vitanda vya wagonjwa, alisema hiyo ni sehemu ya ahadi zake katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Amesema ndani ya miaka mitatu ya kipindi chake cha Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini, amefanya mambo mengi ya kimaendeleo na hata kupitiliza ahadi ambazo alikuwa ameahidi kipindi cha Kampeni kwenye uchaguzi mkuu uliopita 2020, na bado anaendelea kuwatumikia wananchi ikiwamo uboreshaji wa huduma za afya.
“Gari hili la wagonjwa ambalo nalikabidhi ni moja ya vitendea kazi muhimu katika Sekta ya Afya, kwa kubeba wagonjwa na kuwa wahisha kupata huduma za matibabu na kuokoa Afya zao,”amesema Katambi.
Aidha, amesema katika Utawala wake wa Ubunge ataendelea kuboresha upatikanaji wa huduma bora za Afya chini ya Daktari Rais Samia ikiwamo upatikanaji wa Vifaa Tiba, Madawa pamoja na kumalizia ujenzi wa Maboma ya Zahanati ili ya anze kutoa huduma za afya kwa wananchi.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amemshukuru Mbunge huyo kwa kutoa gari la wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, ambayo kwa sasa imefanyiwa maboresho makubwa na gari hilo lilikuwa na uhitaji mkubwa.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk. Elisha Robert, alisema katika Manispaa hiyo uhitaji wa Magari ya wagonjwa ni Manne, kwamba kulikuwa na Magari Mawili lakini Moja liliharibika na kusalia Moja, hivyo kupata gari hiyo imekuwa mkombozi kwa wagonjwa.
Nao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga akiwamo Eliza Masanja, amesema upatikanaji wa Magari ya wagonjwa ni muhimu sana hasa kwa akina Mama Wajawazito, kuwa wahisha kupata huduma za kujifungua kwa uharaka na kuokoa maisha ya Mama na Mtoto.
Aidha, kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa gari la wagonjwa na vitanda, yalitolewa pia Majiko ya Gesi kwa Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Walimu, Wakuu wa Idara na Watumishi wa Afya.










