Ziara hiyo imefanyika Jana ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Shabani Ng'enda, ambayo pia ilitembelea kuona Shimo la uchimbaji wa madini ya Almasi. Ng'enda akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema pomoja na mambo mengine ambayo watakwenda tujadili kwenye Kamati,ameupongeza Mgodi huo wa Mwadui kwamba tangu kutokea tukio la bwawa kubomoka ,wamekuwa pamoja na wananchi na kuwapatia huduma mbalimbali za Kijamii ikiwamo kuwalipa fidia. "Kamati tumetembelea kuona nyumba ambazo Wananchi wamelipwa fidia,na Sisi kama Kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini, tutakwenda kukaa kujadili,wananchi endeleeni kuwa watulivu, tunaupongeza pia Mgodi tangu tukio hili litokee mmekuwa pamoja na wananchi na kuwapatia huduma mbalimbali za kijamii na kuwalipa fidia," amesema Ng'enda.
Aidha, amesema nyumba hizo wameziona ni nzuri na kutoa ushauri zifanyiwe Marekebisho ya kuongezwa Mlango mwingine wa dharura.
Amesema pia wanaitaka Serikali ifanye mapitio upya ya Madhara pamoja na mchakato wa ulipwaji fidia ili kuondoa Manung'uniko yaliyopo kwa baadhi ya wananchi ambao wanaonekana kutoridhika na fidia pamoja na kupewa Elimu namna fidia ilivyofanyika. Naye Diwani wa Mwadui Luhumbo Francis Manyanda, akijibu swali aliloulizwa na Katamati hiyo juu ya wananchi kushirikishwa ulipwaji fidia, amesema kwamba jambo hilo lilikuwa na uwazi na wote wameshirikishwa hadi hatua ya mwisho. Nao baadhi ya wananchi ambao ni wanufaika wa nyumba hizo za fidia akiwamo Suzana Ngussa, amesema wamefarijika kujengewa nyumba hizo imara, na kutoka kuishi kwenye nyumba za tope. Naye Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo, amesema kwamba nyumba za fidia ambazo zilipaswa kujengwa ni 48 na 42 zimekamilika na wananchi wameanza kuishi, mbili ujenzi wake unaendelea,ambapo nyumba Nne wananchi wamegoma wakitaka walipwe fidia ya pesa. Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Shaghembe Mipawa, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo, amesema kwamba tukio hilo la kubomoka Bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui likitokea November 7 Mwaka 2022, na kuathiri wananchi 286 katika Kaya 50 wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze na wamelipwa fidia. Amesema baada ya tukio hilo, walikuwa pamoja na wananchi kwa kuwapatia huduma zote za Kijamii ikiwamo Chakula, Maji, Makazi na Malazi pamoja na Watoto kuwapeleka Shule. Aidha, amesema uzalishaji Rasmi wa Almasi kwenye Mgodi huo ulianza Julai 15 Mwaka Jana, mara baada ya kumalizika kujengwa kwa Bwawa Jipya la kihifadhia Majitope.
Amesema pia Rasilimali za Madini zilizopo kwenye Mgodi huo, zinaweza kuchimbwa zaidi ya miaka 50 Ijayo ikiwa na Carats Milioni 37.46.










