Hakuna usafirishaji haramu wa Watoto na Wenye Ulemavu Namanga -Katambi

04Jan 2024
Na Mwandishi Wetu
ARUSHA
Nipashe
Hakuna usafirishaji haramu wa Watoto na Wenye Ulemavu Namanga -Katambi

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amethibitisha kutokuwepo kwa usafirishaji haramu wa biashara ya binadamu katika mpaka wa Namanga na Kenya hususani kwa watoto na wenye ulemavu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akikagua hali ya utoaji huduma kwa abiria wakiwemo Wenye Ulemavu katika mpaka wa Namanga na Kenya.

Katambi amethibitisha hayo Januari 3, 2023 Jijini Arusha katika Wilaya ya Longido alipofanya ziara katika mpaka wa namanga kwa ajili ya kukagua hali ya utoaji huduma kwa abiria.

 

Amesema taarifa ambazo hivi karibuni zimesambazwa katika mitandao ya kijamii juu ya watoto na wenye ulemavu kusafirishwa kinyume na sheria na kupelekwa nchini kenya kwa ajili ya kutumikishwa zipuuzwe kutokana na hali ya ulinzi na usalama uliopo katika mpaka huo.

Ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kudhibiti vipenyo visivyo halali ikiwa ni pamoja na kuweka polisi jamii ili kuwachukulia hatua watakao bainika wanapita bila kufuata utaratibu

.

Aidha, amesema Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeweka mfumo  wa kielekroniki wa kupata hati ya kusafiria kwa muda mfupi hivyo hakuna sababu ya kusafiri bila kufuata utaratibu.