Hakuna sababu ya vyama vya upinzani kupingana -Zitto

04Jun 2023
Julieth Mkireri
Kagera
Nipashe Jumapili
Hakuna sababu ya vyama vya upinzani kupingana -Zitto

KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema hakuna sababu yoyote ya vyama vya upinzani kuanza kupingana na kukinzana badala yake wanatakiwa kushirikiana katika kuleta mabadiliko.

KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Kiongozi huyo wa Chama ameyasema hayo katika mkutano uliofanyika Bukoba mkoani Kagera ambapo katika mkutano huo mmoja wa wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Azaveli Lwaitama, alisema vyama vyenye malengo sawa havitakiwi kukizana na badala yake kushirikiana kuleta mabadiliko.

"Mnaweza kawa mnapigania jambo moja lakini kila mmoja akapita njia tofauti lakini lengo lenu likiwa ni lilelile, nakushukuru Mzee Lwaitama katika hili ulilolizungumza"

"Inawezekana kabisa watu mkawa mnalengo moja mkapita njia tofauti na hii ni nzuri kila mtu aheshimu njia ya mwenzake ili mradi mfikie lengo badala ya kukozana huku mkiwa na lengo hilo hilo bahati mbaya sana wanasiasa wa Tanzania hiyo hekima haipo" amesema Zitto.