Amesema wanajikita katika kufanya uchunguzi wa kimaabara katika vielelezo mbambali katika masuala ya haki jinai sayansi.
Amebainisha katika maabara za mkemia mkuu wa serikali kuna maabara ya ambayo inachukua vinasaba vya binadamu kwaajili ya kupata matokeo mbalimbali ya uhalifu ikiwemo ubakaji, mauaji na kujeruhiwa.
Vinasaba hivyo vya kisayansi vinatumika katika uchunguzi kutambua muhusika au wahusika ambao wamehusika katika uharifu huo.
Pia ina maabara ya uchunguzi wa matukio yanayohusiana na sumu ambayo imeweza kutumika kumdhulu au kumuua kutambua ni aina gani ya sumu ambayo imetumika
Maabara ingine ni ile ya sayansi kemia ambayo inafanya chunguzi mbalimbali kutambua aina ya dawa za kulevya na uzito au ujazo wa dawa kulevya ambazo zimekamatwa na taasisi mbalimbali zinazohusina na kudhibiti dawa kulevya.
Amebainisha ofisi ya mkemia ina uhisiano wa moja kwa moja na wiki ya sheria kwakuwa wanahusika katika kutoa ushahidi mahakamani wa kisheria.










