Desemba Mosi 2023, Shirika hilo limepanda na kuotesha miti zaidi ya 100 katika shule ya Msingi Msanga Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt.Semistatus Mashimba amehimiza umuhimu wa upandaji miti mashuleni na katika jamii kwa ujumla kwani kufanya hivyo kutadumisha utunzaji wa mazingira na kuondokana na ukame na jangwa.
"Suala la kupanda maua, miti ndio malengo ya Serikali yetu inasisitiza tufanye hivi kila siku na kila mahali, kwani miti inatupa faida ya kivuli na matunda pia” Mashimba.
Afisa Mazingira Halmashauri ya Chamwino, Yustina Ano amesema wanalishukuru shirika hilo kwani limethamini juhudi za utunzaji mazingira.
Amesema katika program hiyo imefanikisha kupanda miti 30 ya matunda ya aina mbalimbali na miche 70 ilioteshwa katika eneo la serikali ya kijiji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Jane Magigita amesema utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja pia wameweza kuzinduzia mashine ya kuchakata mkaa mbadala ili kutunza mazingira.
Amesema mbali na hilo pia EFG wana miradi ya mbalimbali ya kuwawezesha wanawake kiuchumi hususani wanawake waliopo masokoni
Ikiwemo nakuwawezesha wanawake kuwa mabalozi wa kupinga ukatili wa kijinsia.