Lengo likiwa ni kuwawezesha wanafunzi kubuni na kuanzisha mawazo mbalimbali ya kibiasha yatakayowasaidia kuondoa hali ya utegemezi wa ajili ambazo zimekuwa adimu nchini.
Mpango unaojulikana kwa jina la mpango atamizi ‘Incubation’ ni miongoni mwa mipango iliyoandaliwa na chuo hicho ili kuwaanda vijana na wanafunzi wao kujiajili pindi wanapo maliza masomo yao chuoni hapo.
Akizindua mpango Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amekipongeza chuo hicho kwa kuonesha mfano mzuri na kusema kuwa serikali inategemea nguvu kazi ya vijana hususani wale ambao wanapata elimu katika vyuo mbalimbali nchini ikiwa watatumia elimu zao kuliinua taifa kwa kuanzisha mawazo mbalimbali yatakayowezesha kujiajili pamoja na kuwaajili vijana wenzao.
“Unaweza kujiuliza hawa wanasiasi wanatuambia tujiajili mbona wao wapo kazini kwanini wasijiajili, yumekuwa tukikutana na maswali hayo mara kadhaa lakini cha kutambua ni kuwa hata sisi hizi nafasi tulizonazo ni za muda lazima tuwe na maisha nje ya ajila ukipata ajila unaitumikia ukikosa unajiajili mwenyewe,” amesema Masala
Mkurugenzi wa CBE kambasi ya Mwanza Dk.Robert Mashenene amesema mpango huo atamizi unalengo la kuwapa muongozo wa kuanza mapema juhudi za kujenga mawazo yao ya kibiashara kupitia makundi yao waliyoyaanzisha na chuo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha wanayainua mawazo ya wanafunzi hao.
Frank Katumbaku ni mratibu wa mradi huo wa atamizi za kibiashara alisema tayari wamepata wanafunzi watano ambao wanaendelea kuwawezesha katika mawazo yao ya kibunifu katika biashara na tayari wamewasajili na kuwapa mitaji ambapo kila mwaka ni vijana watano wanahitajika ili wezeshwa.
Naye Hawa Hamza ni miongoni mwa wanafunzi wabunifu katika mradi huo amesema mradi huo sio msaada tu kwa vijana hao bali ubunifu wao utasaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.










