Alisema hayo jana alipifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo na baadaye kuzungumza na wazazi katika shule ya Sekondari Chikuyu ambayo ni miongoni mwa shule zilizopata fedha za miradi. Aidha, amewataka walimu na viongozi wa kata kuhakikisha shule zinakuwa na maeneo ya kutosha kulima mazao mbalimbali yatakayowasaidia kupata chakula kwa ajili ya wanafunzi.
Mkuu huyo wa wilay alitembelea miradi ya Ujenzi Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa Mabweni mawili na darasa moja katika shule ya Sekondari Chikuyu, Ukamilishaji wa Bwalo Shule ya Sekondari ya wasichana Solya na ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Kintinku na kuagiza ikamilike haraka.










