Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kulalamikiwa kutoonekana kwenye vikao muhimu na badala yake kukaimisha Maofisa wanaoshindwa kutoa majibu sahihi katika vikao hivyo.
“Kama mnaweza kumtuma Mkurugenzi kwenda China kujifunza kuendesha Halmashauri yenu, basi iwe kwa faida ya Halamshauri, isiwe kichaka cha safari binafsi kutumia fedha za Halmashauri. Kama haikuwa kwa faida ya Halmashauri, fedha zirudishwe.”
“Na hili ninaomba TAKUKURU mfuatilie hiyo safari kama ilikuwa ni kwa maslahi ya Halmashauri na kwamba kuna hela ilitumika kwa maslahi ya Halmashauri kama safari ile haikuwa kwa maslahi ya Halmashauri na zimetumika fedha za Halmashauri kwa maslahi ambayo siyo ya Halmashauri fedha zile zirudishwe zikafanye kazi nyingine.” amesema Mkuu wa Wilaya hiyo.










