"Kumekuwepo na dhana potofu kwa baadhi ya watumishi wa umma, yawezekana kuna mahali nawasumbua lakini ukienda kwenye mamlaka ya utawala huenda ukaona mamlaka yako unanyang'anywa ule umiliki wa miradi....mwaka jana nimewaita wakuu wa shule mara tatu ofsini kwangu,kuwapa maelekezo, mwongozo wa namna ya kutekeleza miradi kwa ufanisi pamoja na kuwasaidia pale nilipoona wamekwama".
"Miongoni mwao walinyanyuka na kuanza kupiga simu kwa mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wa juu kuwa DC anatuingilia kwenye miradi...kazi ya DC ni kuisaidia halmashauri kutekeleza majukumu yake, kupewa fedha kama wewe ni mkuu wa kituo cha afya,Mwalimu mkuu, au mkuu wa idara frani haikupi uhuru mkubwa kuwa una mamlaka ya kutohojiwa na mtu yoyote hapana na siyo kweli...lazima tutaendelea kukusimamieni,kukuelezeni na kukushaurini" amesema Katwale.
Ameithibitisha Nipashe Digital kuwa hatorudi nyuma katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, na kwamba ataendelea kukemea na kuonya pale panapostahili pasipo kumwonea haya mtumishi yeyote kwa kuwa serikali ya awamu ya sita inakusudia kuondoa adha za muda mrefu ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi.










