Boss afutwa kazi kisa umeme kukatika

27Aug 2023
Nairobi
Nipashe Jumapili
Boss afutwa kazi kisa umeme kukatika

MKUU wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini Kenya, Alex Gitari amefutwa kazi baada ya kukatika kwa umeme na kuwaacha abiria wakiwa gizani kwa saa kadhaa katika Uwanja Mkuu wa Ndege wa Nairobi.

Alex Gitari.

Alex Gitari alifutwa kazi na Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen, ambaye ameomba radhi kwa changamoto hiyo iliyotokea.

Kampuni kubwa ya umeme inayomilikiwa na Serikali haijaeleza ni nini hasa kilichosababisha kukatika kwa umeme nchini kote. Ingawa baadhi ya maeneo umeme umeanza kujeshwa.

Aidha, Waziri wa Usafiri nchini humo amesema kuwa uwanja huo wa ndege una miliki majenereta mawili yaliyonuniliwa miaka kadhaa iliyopita lakini hayajaunganishwa.