Binti wa miaka 24 ashinda ubunge Kenya

14Aug 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Binti wa miaka 24 ashinda ubunge Kenya

BINTI wa miaka 24 Linet Toto, ametangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Kenya kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa Viti Maalumu kwenye Kaunti ya Bomet akiwashinda wagombea wengine wanane kwenye kinyang’anyiro hicho.

Toto ambaye kwa mara ya kwanza amegombea nafasi hiyo kupitia chama cha UDA ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 242,775 na kumfanya kuwa mwanasiasa mdogo zaidi kujiunga na Bunge la 13.

Mbunge mteule huyo, ametaja ukosefu wa fedha kwenye kampeni zake kama changamoto kubwa aliyokumbana nayo.

“Sikuwa na fedha ya kufanya kampeni maana mimi nimetoka kuhitimu elimu yangu ya chuo hivi karibu na hicho ndio kilikuwa kikwazo changu kwenye uchaguzi wa mwaka huu,”amesema.