Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Lucas Mwakatundu, alimtaja aliyefariki dunia ni Alon Basili (36), mkazi wa Kijiji cha Mkiwa ambaye mwili wake umehifadhiwa katika Zahanati ya Ikungi.
Alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:20 usiku katika Kijiji cha Mkiwa wilayani Ikungi mkoani Singida barabara kuu ya Dodoma-Singida na kulitaja basi hilo ni lenye namba za usajili T 417 CTD aina ya Scania.
Kamanda Mwakatundu aliwataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Martha Jeremiah (36), mkazi wa Kijiji cha Mkiwa na Nassoro Abdallah (11), mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkiwa.
Alisema wakati ajali hiyo ikitokea, majeruhi wote walikuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo na kwa sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Gasper iliyoko Itigi Wilaya ya Manyoni.
Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na Jeshi la Polisi linamshikilia, Boniphace Machage ambaye ni dereva wa basi hilo kwa uchunguzi zaidi.










