Kadhalika, kimeiomba Tume ya Uchaguzi zanzibar (ZEC) kusimamia kwa haki uchaguzi huo ili kuhakikisha unafanyika kwa uhuru, usalama na utulivu.
Mshauri na Mlezi wa ADC, Hamad Rashid Mohamed, alisema jana jijini Dar es Salaam jana kuwa maandalizi ya chama hicho ya kushiriki katika uchaguzi huo yamekamilika.
Hamad ambaye ni mgombea urais kupitia chama hicho, alishauri ZEC kuhakikisha inaepuka kurudia makosa yaliyotokea katika uchaguzi wa Octoba 25, mwaka jana, kwa kuwa inaweza kuleta matatizo zaidi.
Pia alishauri vyombo vya ulinzi na usalama visiwani humo kuhakikisha vinatenda haki na kuzingatia maadili ya kazi yake ikiwamo kuimarisha ulinzi siku ya uchaguzi.
Pia alivitaka vyama vya siasa kutokuwa chachu ya kuchochea vurugu katika uchaguzi huo na badala yake vihakikishe vinawaelimisha watu wake kuimarisha amani na utulivu siku hiyo.
ZEC ilitangaza kurudiwa uchaguzi huo Machi 20, mwaka huu, baada ya kufutwa kwa ule uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.










