ACT yatoa msimamo muhimu Z'bar

07May 2016
Mwinyi Sadallah
Zanzibar
Nipashe
ACT yatoa msimamo muhimu Z'bar

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimetangaza kumtambua Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na serikali yake baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20.

Uchaguzi huo uliacha mpasuko wa kisiasa kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Akitangaza msimamo huo, Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ramadhan Suleiman Ramadhan alisema hakuna sababu ya kukwepa kuitambua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu kila mwananchi analipa kodi na kupokea huduma za kijamii kutoka serikalini.

Kutokuitambua, alisema, ni mbwembwe za kisiasa. CUF imetangaza kutotambua.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha usafi wa mazingira wa nyumba za kulelea wazee wasiojiweza, Ramadhani alisema Chama chake kitafanya kazi bega kwa bega na Serikali katika kusukuma maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake.

“Serikali ikifanya vizuri tutaisaidia na ikifanya vibaya tutaikosoa, lengo ni kuwatumikia wananchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa,” alisema.

Usafi huo wa nyumba za kulelea wazee ilikuwa ni maadhimisho ya miaka miwili tangu kuzaliwa kwa chama hicho.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umekamilika hivyo kazi iliyopo mbele kwa chama kilichoshinda ni kuhakikisha kinatekeleza utatuzi wa kero za wananchi na kufanikisha mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Kiongozi huyo alisema Chama hicho hakijawahi kufanya kikao chochote cha kutoitambua SMZ mbali ya kujadili hali ya kisiasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao ulifutwa matokeo na kurudiwa Machi 20.

“ACT Wazalendo tulishiriki uchaguzi wa marudio baada ya majadiliano ya kina pamoja na mgombea wetu kutofikia malengo," alisema Ramdhani.

"Kazi iliyopo mbele yetu sasa kama Chama cha Siasa kujenga nchi kwa kutumia sauti ya demokrasia na tutaisimamia serikali na kuikosoa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.”

Ali Mohamed Shein umeonesha nia njema hasa katika kupambana na tatizo la ufisadi, rushwa, kukosekana
Msimamo wa kutoitambua SMZ ulitangazwa na CUF baada ya kususia uchaguzi mkuu wa marudio, wakipinga kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kwa madai ulikuwa huru na wa haki.